UTANGULIZI
Kwa mujibu wa Kamusi
ya Kiswahili Sanifu,Toleo la pili(2004) neno’MSINGI”
nm (mi-) Inamaanisha mahali palipochimbwa
na kujengwa imara kwa madhumuni ya kusimamisha jengo.
Hivyo basi,tukihawilisha
maana hiyo katika dhana ya misingi ya kubuni,kufaragua na kutengeneza zana za
ufundishaji na ujifunzaji;
Misingi ya kubuni na
kufaragua V/T ni mambo muhimu ya kuzingatia kama mwalimu unapokuwa katika zoezi
zima la kubuni,kufaragua na kutengeneza zana mbalimbali za ufundishaji na
ujifunzaji.Ili zana itakayotengenezwa iwe bora,imara na kuleta ufanisi katika
swala zima la ufundishaji na ujifunzaji.
Mambo hayo ndiyo
yatakayodhihirisha kama vielelezo ama zana zote zilizobuniwa,faraguliwa na zilizotengenezwa zimekidhi vigezo vinavyokubaliwa ama hazikidhi.
Misingi hii,hutoa
taswira ya zana itakayotengenezwa kabla
ya zoezi la kubuni,kufaragua na kutengeneza V/t MBALIMBALI,hivyo mwalimu hana
budi kuzingatia misingi hiyo pindi anapokuwa katika zoezi zima la kuandaa vielelezo na teknolojia mbalimbali za
ufundishaji na ujifunzaji.
Katika somo letu la
vielelezo na teknolojia kuna misingi mikuu sita(6) ambayo huna budi kuizingatia
wakati wa zoezi zima la kubuni,kufaragua na kutengeneza vielelezo na teknolojia
mbalimbali za kufundushia na kujifunzia ambayo ni;
1.
Uelewaji wa lengo mahususi
2.
Uzingatiaji wa umri na uelewa wa walengwa
3.
Uchoraji wa michoro na vipimo
4.
Uzingatiaji wa ubora wa vielelezo na
teknolojia
5.
Udadisi na ufikirishaji kwa mlengwa
6.
Uhusiano wa vielelezo na teknolojia na mada
husika
A) UELEWAJI
WA LENGO MAHUSUSI
Katika msingi huu,unapokuwa katika zoezi
zima la kubuni,kufaragua na kutengeneza zana mbalimbali za ufundishaji na
ujifunzaji, zana hizo ni lazima ziendana
na malengo mahusi ya somo na si vinginevyo.Mfano,unafundisha mada ya mawasiliano
katika somo la Tehama,hivyo basi zana hiyo iendane na malengo mahusi ya somo
kwa siku hiyo ili ieleweke kwa urahisi kwa wanafunzi na kutotoka nje ya malengo
ya somo.
B) UZINGATIAJI
WA UMRI NA UELEWA WA WALENGWA
Zana zitakazotengenezwa sharti ziendane na
umri na uelewa wa walengwa/wanafunzi.Mfano zana ya mwanafunzi wa darasa la
tatu na
ya mwanafunzi wa darasa la 7 zitatofautiana kulingana na umri na uelewa
wa wanafunzi hao hata kama mada watayofundishwa itakuwa ni moja ama ya kufanana.Mwalimu hana budi kuzingatia kigezo hiki ili zana
utakayoitengeneza ieleweke kwa urahisi na kufanikisha malengo ya somo lake.
C) UCHORAJI
WA MICHORO NA VIPIMO.
Michoro mbalimbali iliyobuniwa,faraguliwa na
kutengezwa sharti iwe na vipimo sahihi ili iweze kueleweka,kuonekana kwa
urahisi na kufanikisha malengo ya ufundishaji na ujifunzaji.
Mfano unapochora umbo la pembe tatu,sharti
uwe na vipimo maalumu ili vikizi vigezo na si kuchora tuu,ili michoro yetu iweze kuonekana na kueleweka kwa urahisi.
D) UZINGATIAJI
WA UBORA WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA.
Vielelezo/zana zitakazotengenezwa sharti
ziwe bora na imara ili ziweze kutumika kwa muda mrefu.Pia kukupunguzia gharama
ya kuvitengeza mara kwa mara.
E) UDADISI
NA UFIKIRISHAJI KWA WALENGWA
Zana itakayotengenezwa sharti ikuze udadisi
na ufikirishaji kwa walengwa.Zana inaweza ikakuza udadisi kama haitataja mambo
kwa waziwazi ili kumpa nafasi mlengwa kudadisi na hatimaye kupata
jawabu.Ileweke kuwa kazi ya mwalimu katika ulimwengu huu wa njia shirikishi za
ufundishaji ni kuwaongoza wanafunzi na
si kuonyesha kama wewe ndiye unayejua kila kitu au kila jambo.Kwa mfano,upi katika
michoro ifuatayo,unaweza kukuza udadisi na ufikirishaji
kwa walengwa?.
F) UHUSIANO
WA V/T NA MADA HUSIKA
Hapa zana itakayotengenezwa sharti iendane
na mada husika ya somo.Utofauti wa msingi huu na ule wa kwanza ni kama zana za
mada zinaweza zikawa nyingi kwani zana hizo huwa zinaandaliwa kukidhi mada
nzima,wakati zana yenye kulenga malengo
mahususi zitakidhi malengo mahususi tuu.Ama kwa namna nyingine, ndani ya mada
kuna mada ndogo ndogo ambazo ndizo zitakazopelekea mwalimu kuanda zana
kulingana na malengo mahususi ya somo.Kuelewa dhana hii kwa undani,zingatia
namna unavyoandika zana katika AZIMIO LA KAZI NA ANDALIA LA SOMO.
Vizur xnaa
ReplyDelete