WELCOME NOTE

WELCOME NOTE

PICHA

PICHA

TANGAZO

Thursday, November 15, 2012

AINA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA


      Vielelezo na teknolojia kwa ufundishaji na ujifunzaji vimegawanyika katika aina kuu mbili.

1                   Vielelezo na teknolojia asilia

2           Vielelezo na teknolojia kisasa

a)      VIELELEZO NA TEKNOLOJIA ASILIA
Ina maana ya zana au vifaa rahisi ambavyo huweza kupatikana au kutengenezwa katika mazingira alimo mwalimu na wanafunzi kwa kutumia vitu vilivyomo katika mazingira yao.Mfano,vitu halisi kama vile matunda,samani,mimea,viumbe hai,nk.
Vifaa vya  maumbo mbalimbali pia huweza kutengenezwa kama vile vifani vya viumbe hai,maumbo yenye ukumbi kama vik mche duara,mche mstatili,tufe nk.

                SIFA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA ASILIA
         i.                                     
                           Vinapatikana kwa urahisi
       ii.                                           Havina gharama kubwa
      iii.                                          Havihitaji maarifa ya ziada katika kuvitumia
     iv.                                            Havitumii nishati ya umeme
      
     vi.                                         Utengenezaji wake hujikita au hutokana na vitu vinavyopatikana katika mazingira aliyomo mwalimu 
                          na mwanafunzi

           b)      VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KISASA

Hizi ni zana au vifaa vya kisasa ambavyo ni vigeni na havijazoeleka katika kuvitengeza au kuvitumia.
Zana au vifaa hivi ni kama vile matumizi ya video,runinga,filamu,projekta na kompyuta

SIFA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KISASA
                                                         i.            Vina gharama
                                                       ii.            Vinahitaji nishati ya umeme
                                                      iii.            Vinahitaji maarifa na ujuzi wa kuvitumia
                                                     iv.            Havipatikani kwa urahisi
                                                       v.            Ni vigeni katika mazingira ya mwalimu na mwanafunzi
                                                     vi.            Vinatumia sayansi na teknolojia ya hali ya juu katika matumizi yake.


Wednesday, October 17, 2012

MATUKIO KATIKA PICHA:WANACHUO WAKIWA WANAFAFANUA,NAMNA WALIVYOFARAGUA NA KUTENGENEZA ZANA MBALIMBALI ZA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI

KWA KUTUMIA MAKUNZI YANAYOPATIKANA KATIKA MAZINGIRA YA CHUO CHA UALIMU MHONDA.
 Wanachuo wa 2A3 2011/2102 ,wakionyesha mfano wa Treka waliotengeneza kwa kutumia BATI,BOKSI,VIBAO,NA VIPANDE VYA NDALA VILIVYOPATIKANA KATIKA MAJALALA YA CHUO,NA KISHA KUPAKA RANGI, ILI KUVUTIA NA KULETA UHALISIA WA KITU HALISI.
WAFARAGUZI WAKITOA MAELEKEZO YA HATUA WALIZOZIFUATA KTK KUBUNI,KUFARAGUA NA KUTENGENEZA ZANA YAO

WAFARAGUZI WAKIONYESHA ZANA YAO DARASANI NA KUTOA UFAFANUZI WA NAMNA WALIVYOTENGENEZA.
HII NI PICHA YA MONITOR YA KOMPUTA ILIYOTENGENEZWA KWA KUTUMIA BOKSI KISHA KUPAKWA RANGI ZILIZOPELEKEA KULETA UHALISIA WA ZANA HUSIKA.
 MFARAGUZI AKIWA KATIKA MATAYARISHO YA MWISHO YA KUKAMILISHA ZANA TAYARI KUIWASILISHA ZANA HII DARASANI KWA UFAFANUZI ZAIDI.
MFARAGUZI AKIWA KATIKA MATAYARISHO YA MWISHO YA KUKAMILISHA ZANA YAKE ALIYOIFARAGUA KWA KUTUMIA MAKUNZI RAHISI YANAYOPATIKANA KATIKA MAZINGIRA YA CHUO CHA UALIMU MHONDA.

Monday, September 24, 2012

VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA


                   2.1 Vielezo na teknolojia kwa kufundishia na kujifunzia
                   2.2 Upatikanaji wa vielelezo na teknolojia                    
 
DHANA NA MAANA YA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA

Ni jumla ya zana au vifaa ikiwa ni asilia au vya kisasa vinavyoweza kutumiwa na mwalimu katika ufundishaji na kumsaidia kufundisha mada husika kwa ufanisi zaidi na mwanafunzi kuelewa mada hiyo kwa urahisi.
Mfano tufe,matunda,komputa,redio,projecta,vifani mbalimbali nk.
 
 SIFA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
i.                  Viwe sahihi katika muundo wake na kwa matumizi. Hii ina maana iwe na mjengo uliorahisi kuonekana, kupangwa na kupanguliwa
ii.         Viwe na ukubwa unaofaa. Hii ina maana zana iwe na ukubwa wa kati, kama ni chombo cha sauti, pia kiwe na sauti ya kati
iii.        Viwe na mvuto,ili kuvuta usikivu kwa walengwa.
iv.        Vishabihiane na ujumbe uliokusudiwa
v.         Vizingatie umri na uelewa wa walengwa
vi.        Viwe imara na vya kudumu
vii.       Visiwe na uwezo wa kupotosha dhana iliyokusudiwa
viii.      Viendane na mazingira halisi ya watoto
ix.        Vihamishike/viwe rahisi kubebeka.
NJIA ZA UPATIKANAJI WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA 
Vielelezo vya kufundishia na kujifunzia vinaweza kupatikana katika njia kuu zifuatazo:
                                                                                i.            Kununuliwa.Mfano: Komputa,magazeti,redio,tepurekoda,projekta nk
                                                                               ii.            Kuazima.Mfano:-Kompyuta,projekta nk.
                                                                             iii.            Kuchukua/kutayarishwa kutoka mahali vilipohifadhiwa
                                                                             iv.            Kutengenezwa/kufaraguliwa,kama vile:-vifani vya viumbe hai,maumbo yenye ukumbi kama vile mche duara,mche mstatili,tufe nk.

Friday, September 14, 2012

MISINGI YA KUBUNI, KUFARAGUA NA KUTENGENEZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA


UTANGULIZI

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu,Toleo la pili(2004) neno’MSINGI” nm (mi-) Inamaanisha mahali palipochimbwa na kujengwa imara kwa madhumuni ya kusimamisha jengo.
Hivyo basi,tukihawilisha maana hiyo katika dhana ya misingi ya kubuni,kufaragua na kutengeneza zana za ufundishaji na ujifunzaji;
Misingi ya kubuni na kufaragua V/T ni mambo muhimu ya kuzingatia kama mwalimu unapokuwa katika zoezi zima la kubuni,kufaragua na kutengeneza zana mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji.Ili zana itakayotengenezwa iwe bora,imara na kuleta ufanisi katika swala zima la ufundishaji na ujifunzaji.
Mambo hayo ndiyo yatakayodhihirisha kama vielelezo ama zana zote zilizobuniwa,faraguliwa na  zilizotengenezwa zimekidhi vigezo  vinavyokubaliwa ama hazikidhi.
Misingi hii,hutoa taswira ya zana itakayotengenezwa  kabla ya zoezi la kubuni,kufaragua na kutengeneza V/t MBALIMBALI,hivyo mwalimu hana budi kuzingatia misingi hiyo pindi anapokuwa katika zoezi zima la kuandaa  vielelezo na teknolojia mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji.
Katika somo letu la vielelezo na teknolojia kuna misingi mikuu sita(6) ambayo huna budi kuizingatia wakati wa zoezi zima la kubuni,kufaragua na kutengeneza vielelezo na teknolojia mbalimbali za kufundushia na kujifunzia ambayo ni;
1.       Uelewaji wa lengo mahususi
2.       Uzingatiaji wa umri na uelewa wa walengwa
3.       Uchoraji wa michoro na vipimo
4.       Uzingatiaji wa ubora wa vielelezo na teknolojia
5.       Udadisi na ufikirishaji kwa mlengwa
6.       Uhusiano wa vielelezo na teknolojia na mada husika

     A)     UELEWAJI WA LENGO MAHUSUSI
Katika msingi huu,unapokuwa katika zoezi zima la kubuni,kufaragua na kutengeneza zana mbalimbali za ufundishaji na ujifunzaji,  zana hizo ni lazima ziendana na malengo mahusi ya somo na si vinginevyo.Mfano,unafundisha mada ya mawasiliano katika somo la Tehama,hivyo basi zana hiyo iendane na malengo mahusi ya somo kwa siku hiyo ili ieleweke kwa urahisi kwa wanafunzi na kutotoka nje ya malengo ya somo.
 
     B)      UZINGATIAJI WA UMRI NA UELEWA WA WALENGWA
Zana zitakazotengenezwa sharti ziendane na umri na uelewa wa walengwa/wanafunzi.Mfano zana ya mwanafunzi wa darasa la tatu  na  ya mwanafunzi wa darasa la 7 zitatofautiana kulingana na umri na uelewa wa wanafunzi hao hata kama mada watayofundishwa itakuwa ni moja ama  ya kufanana.Mwalimu  hana budi kuzingatia kigezo hiki ili zana utakayoitengeneza ieleweke kwa urahisi na kufanikisha malengo ya somo lake.

     C)      UCHORAJI WA MICHORO NA VIPIMO.
Michoro mbalimbali iliyobuniwa,faraguliwa na kutengezwa sharti iwe na vipimo sahihi ili iweze kueleweka,kuonekana kwa urahisi na kufanikisha malengo ya ufundishaji na ujifunzaji.
Mfano unapochora umbo la pembe tatu,sharti uwe na vipimo maalumu ili vikizi vigezo na si kuchora tuu,ili michoro yetu iweze kuonekana na kueleweka kwa urahisi.

 
     D)     UZINGATIAJI WA UBORA WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA.
Vielelezo/zana zitakazotengenezwa sharti ziwe bora na imara ili ziweze kutumika kwa muda mrefu.Pia kukupunguzia gharama ya kuvitengeza mara kwa mara.

     E)      UDADISI NA UFIKIRISHAJI KWA WALENGWA
Zana itakayotengenezwa sharti ikuze udadisi na ufikirishaji kwa walengwa.Zana inaweza ikakuza udadisi kama haitataja mambo kwa waziwazi ili kumpa nafasi mlengwa kudadisi na hatimaye kupata jawabu.Ileweke kuwa kazi ya mwalimu katika ulimwengu huu wa njia shirikishi za ufundishaji  ni kuwaongoza wanafunzi na si kuonyesha kama wewe ndiye unayejua kila kitu au kila jambo.Kwa mfano,upi katika michoro ifuatayo,unaweza kukuza udadisi na ufikirishaji kwa walengwa?.
 
     F)      UHUSIANO WA V/T NA MADA HUSIKA
Hapa zana itakayotengenezwa sharti iendane na mada husika ya somo.Utofauti wa msingi huu na ule wa kwanza ni kama zana za mada zinaweza zikawa nyingi kwani zana hizo huwa zinaandaliwa kukidhi mada nzima,wakati zana  yenye kulenga malengo mahususi zitakidhi malengo mahususi tuu.Ama kwa namna nyingine, ndani ya mada kuna mada ndogo ndogo ambazo ndizo zitakazopelekea mwalimu kuanda zana kulingana na malengo mahususi ya somo.Kuelewa dhana hii kwa undani,zingatia namna unavyoandika zana katika AZIMIO LA KAZI NA ANDALIA LA SOMO.