2.1 Vielezo na teknolojia kwa kufundishia na kujifunzia
2.2 Upatikanaji wa vielelezo na
teknolojia
DHANA NA MAANA YA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
Ni jumla ya zana au vifaa ikiwa ni asilia au vya kisasa
vinavyoweza kutumiwa na mwalimu katika ufundishaji na kumsaidia kufundisha mada
husika kwa ufanisi zaidi na mwanafunzi kuelewa mada hiyo kwa urahisi.
Mfano tufe,matunda,komputa,redio,projecta,vifani mbalimbali nk.
SIFA ZA VIELELEZO NA
TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
i. Viwe
sahihi katika muundo wake na kwa matumizi. Hii ina maana iwe na mjengo
uliorahisi kuonekana, kupangwa na kupanguliwa
ii. Viwe
na ukubwa unaofaa. Hii ina maana zana iwe na ukubwa wa kati, kama
ni chombo cha sauti, pia kiwe na sauti ya kati
iii. Viwe
na mvuto,ili kuvuta usikivu kwa walengwa.
iv. Vishabihiane
na ujumbe uliokusudiwa
v. Vizingatie
umri na uelewa wa walengwa
vi. Viwe
imara na vya kudumu
vii. Visiwe
na uwezo wa kupotosha dhana iliyokusudiwa
viii. Viendane
na mazingira halisi ya watoto
ix. Vihamishike/viwe rahisi kubebeka.
NJIA
ZA UPATIKANAJI WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
Vielelezo
vya kufundishia na kujifunzia vinaweza kupatikana katika njia kuu zifuatazo:
i.
Kununuliwa.Mfano:
Komputa,magazeti,redio,tepurekoda,projekta nk
ii.
Kuazima.Mfano:-Kompyuta,projekta nk.
iii.
Kuchukua/kutayarishwa kutoka mahali
vilipohifadhiwa
iv.
Kutengenezwa/kufaraguliwa,kama vile:-vifani vya
viumbe hai,maumbo yenye ukumbi kama vile mche duara,mche mstatili,tufe nk.