WELCOME NOTE

WELCOME NOTE

PICHA

PICHA

TANGAZO

Tuesday, April 16, 2013

UMUHIMU WA KUFANYA MAJARIBIO YA ZANA KABLA YA KUZITUMIA DARASANI


Ni jambo la busara kwa mwalimu kuvifanyia vielelezo majaribio kabla ya kuvitumia.
Hatua hii humwezesha kufanya yafuatayo:-
a)     Kuona kama zana/ vifaa ni vizima au ni vibovu viweze kutengenezwa/ kununua/ kutafuta vingine.
b)     Kuhakikisha kama zana/ vifaa hivyo vinafanya kazi kwa usahihi kama vilivyokusudiwa
c)     Kujiamini katika kufundisha hatua anuai za somo lake na kutumia vielelezo vyake
d)     Kujua uthabiti na udhaifu wa vielelezo vyenyewe
e)     Kuhakikisha kwamba havijaharibika, na kama vimeharibika aweze kuandaa vingine kabla ya siku ya somo lenyewe
f)       Kufahamu madhara yanayoweza kuletwa na vielelezo hivyo mfano:- Tindikali  n.k.
g)     Kufahamu namna ya kutumia vielelezo hivyo.

VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA WENYE MAHITAJI MAALUMU


Mtoto wenye mahitaji maalumu:- Ni yule ambaye ama ana uwezo mkubwa kuliko wanafunzi wote wa kawaida au uwezo wake wa kujifunza na kuelewa ni mdogo sana au ana dosari katika maumbile yake. Mwalimu ataweza kutambua mtoto mwenye mahitaji maalumu kwa kuona kuwa matendo ni tofauti na watoto wengine. Hivyo basi mwalimu lazima awe na upeo na saikolojia kubwa ya kumwezesha kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu katika darasa lake.
Mfano wa  watoto wenye mahitaji maalumu ni:-
          Watoto wenye mtindio wa ubongo (taahira)
          Wasiiona (vipofu)
      Wasiosikia (viziwi)
          Wasiosema (bubu)
          Walemavu wa viungo vya mwili (vilema)
      Watoto wenye vipaji maalumu

(a) KUNDI LA WASIOONA
Kundi hili hujumuisha watoto wenye uoni hafifu ambao wanaweza kutumia vielelezo vya watu wa kawaida
Mwalimu anapaswa kuwawekea watoto wa namna hii karibu na ubao, kama utatumia michoro, picha sanjari na maandishi, yanalazimika yawe ni yenye kuonekana au maandishi yawe yaliyokuzwa.
Aina ya pili ya wasioona ni wale kusikia, kugusa, kunusa au kuonja. Hivyo basi vielelezo vifuatavyo vinaweza kutumika:-
  • Vitu halisi (kugusa, kuonja na kunusa)
  • Vinasa sauti/ tepurekoda (vielelezo na teknolojia masikizi).
  • Maandishi ya nukta nundu/ maandishi ya wasioona

(b) KUNDI LA WASIOSIKIA
Watu wa namna hii wamegawanyika katika makundi mawili. Wenye uwezo mdogo wa kusikia na wasiosikia kabisa. Wenye mdogo wa kusikia mwalimu anapaswa kuweka mbele ya darasa na kwa wale wasiosikia kabisa vielelezo na teknolojia vifuatavyo vinaweza kutumika:-
  • Vielelezo na teknolojiamaono (Picha, chati,  n. k)
  • Vitu halisi (wataona, watagusa na kuonja)
  • Lugha ya alama kwa wasiosikia
  • Kufuatisha mdomo (lips reading)

© KUNDI LA WASIOSEMA WALA KUSIKIA
Watu ambao hawana uwezo wa kusema wala kusikia, mwalimu anashauriwa kutumia vielelezo vifuatavyo:-
  • Lugha ya ishara
  • Vitu halisi kama vile miti, matunda, wanyama  n.k.
  • Picha mbalimbali Mfano, za wanyama, watu, mimea  n.k.

TANBIHI:- Watu kama wenye vipaji maalumu, walemavu wa miguu na wenye mtindio wa ubongo, Vilelelezo vinavyoweza kutumika kwa watu hawa vitawiana

UTUNZAJI WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA


Dhana.
Ni hali ya kuweka vielelezo katika mazingira sahihi na yaliyo mazuri au salama ili kuhifadhi kutokana na uharibifu wa aina yoyote ule.

 Waharibifu wa vielelezo.
Waharifu wa vielelezo vya kufundishia/ kujifunzia ni wengi ikiwa ni pamoja na mikono ya watu wenyewe. Waharibifu wengine ni hali ya hewa, upepo, vumbi, wadudu waharibifu n. k.

Hali ya hewa
Ni moja kati ya waharibifu wa zana au vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Athari zinazosababishwa na hali ya hewa ni kubabuka rangi kwa chati au picha inapobandikwa kwa muda mrefu hupoteza nuru ya rangi.
Aidha hali ya hewa baridi husababisha ukungu kwenye vifaa ambavyo havikuhifadhiwa vizuri mfano kanda za video, kanda za kinasa sauti  n.  k. Hivyo basi mara baada ya kutumika mwalimu anatakiwa kuvihifadhi ili visiharibike.

Upepo na vumbi
Upepo unapeperusha chati na picha zilizopachikwa ukutani na juu ya ubao husababisha kuchanika. Upepo pia hupeperusha vumbi ambalo huaribu vitu kama vide, redio, kanda za sauti  n. k. Iwapo vifaa hivi havikuhifadhiwa vizuri vinaweza kuharibika.

Wadudu waharibifu
Mfano mchwa, mende, panya  n.k.Mwalimu analazimika awe muangalifu sana juu ya wadudu hawa kwani ni wadudu hatari sana kwa kuharibu zana za kufundishia.

 NJIA ZA UTUNZAJI WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA
Katika utunzaji wa vielelezo na teknolojia kwa kufundishia/ kujifunzia. Vielelezo vinaweza kugawanyika katika makundi mawili (2)
(i)                  Vinavyowekeka kwa muda mrefu
(ii)                Vinavyowekeka kwa muda mfupi

Vinavyowekeka kwa muda mfupi ni kama:- matunda, dagaa, aina mbalimbali za mboga za majani, hizi hutumika kwa muda mfupi na kutupwa jalalani na vile vinavyowekeka kwa muda mrefu, viwekwe kwa utaratibu mzuri ili visiharibike
 Njia zifuatazo zinaweza kutumika katika kuhifadhi vielelezo:-
(i)                  kuhifadhi katika visanduku au masanduku maalumu.
(ii)                Kuviweka katika kabati kutokana na wadudu waharibifu
(iii)               Kuviweka katika mifuko ya plastiki na kufungwa vizuri ili hewa isipite ambayo hatimaye huenda ikasababisha uharibifu
(iv)             Kutumia mikebe isiyopenyeza hewa. Hii inaweza kuhifadhi lenzi za projekta au projekta yenyewe na vitu vidogovidogo vinavyoharibika kwa ukungu vihifadhiwe katika mikebe hiyo au katika mikoba yao
(v)               Kuvisafisha na kuviangalia mara kwa mara
(vi)             Njia ya kugandishwa kwenye karatasi ngumu na kufanya fremu kwa mfano chati au picha zilizochorwa kwenye karatasi nyepesi zinaweza kubandikwa, kuninginizwa juu ya ukuta wa darasa
(vii)            Kuviweka katika chumba maalumu.
(viii)          Vipangwe vizuri ili visigongane au kujeruhiana.

Thursday, November 15, 2012

AINA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA


      Vielelezo na teknolojia kwa ufundishaji na ujifunzaji vimegawanyika katika aina kuu mbili.

1                   Vielelezo na teknolojia asilia

2           Vielelezo na teknolojia kisasa

a)      VIELELEZO NA TEKNOLOJIA ASILIA
Ina maana ya zana au vifaa rahisi ambavyo huweza kupatikana au kutengenezwa katika mazingira alimo mwalimu na wanafunzi kwa kutumia vitu vilivyomo katika mazingira yao.Mfano,vitu halisi kama vile matunda,samani,mimea,viumbe hai,nk.
Vifaa vya  maumbo mbalimbali pia huweza kutengenezwa kama vile vifani vya viumbe hai,maumbo yenye ukumbi kama vik mche duara,mche mstatili,tufe nk.

                SIFA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA ASILIA
         i.                                     
                           Vinapatikana kwa urahisi
       ii.                                           Havina gharama kubwa
      iii.                                          Havihitaji maarifa ya ziada katika kuvitumia
     iv.                                            Havitumii nishati ya umeme
      
     vi.                                         Utengenezaji wake hujikita au hutokana na vitu vinavyopatikana katika mazingira aliyomo mwalimu 
                          na mwanafunzi

           b)      VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KISASA

Hizi ni zana au vifaa vya kisasa ambavyo ni vigeni na havijazoeleka katika kuvitengeza au kuvitumia.
Zana au vifaa hivi ni kama vile matumizi ya video,runinga,filamu,projekta na kompyuta

SIFA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KISASA
                                                         i.            Vina gharama
                                                       ii.            Vinahitaji nishati ya umeme
                                                      iii.            Vinahitaji maarifa na ujuzi wa kuvitumia
                                                     iv.            Havipatikani kwa urahisi
                                                       v.            Ni vigeni katika mazingira ya mwalimu na mwanafunzi
                                                     vi.            Vinatumia sayansi na teknolojia ya hali ya juu katika matumizi yake.