Mtoto wenye
mahitaji maalumu:-
Ni yule ambaye ama ana uwezo mkubwa kuliko wanafunzi wote wa kawaida au uwezo
wake wa kujifunza na kuelewa ni mdogo sana
au ana dosari katika maumbile yake. Mwalimu ataweza kutambua mtoto mwenye
mahitaji maalumu kwa kuona kuwa matendo ni tofauti na watoto wengine. Hivyo
basi mwalimu lazima awe na upeo na saikolojia kubwa ya kumwezesha kuwatambua
watoto wenye mahitaji maalumu katika darasa lake.
Mfano
wa watoto wenye mahitaji maalumu ni:-
Watoto
wenye mtindio wa ubongo (taahira)
Wasiiona
(vipofu)
Wasiosikia
(viziwi)
Wasiosema
(bubu)
Walemavu
wa viungo vya mwili (vilema)
Watoto
wenye vipaji maalumu
(a) KUNDI LA
WASIOONA
Kundi
hili hujumuisha watoto wenye uoni hafifu ambao wanaweza kutumia vielelezo vya
watu wa kawaida
Mwalimu
anapaswa kuwawekea watoto wa namna hii karibu na ubao, kama
utatumia michoro, picha sanjari na maandishi, yanalazimika yawe ni yenye
kuonekana au maandishi yawe yaliyokuzwa.
Aina
ya pili ya wasioona ni wale kusikia, kugusa, kunusa au kuonja. Hivyo basi vielelezo
vifuatavyo vinaweza kutumika:-
- Vitu halisi (kugusa, kuonja na kunusa)
- Vinasa sauti/ tepurekoda (vielelezo na teknolojia masikizi).
- Maandishi ya nukta nundu/ maandishi ya wasioona
(b)
KUNDI LA WASIOSIKIA
Watu
wa namna hii wamegawanyika katika makundi mawili. Wenye uwezo mdogo wa kusikia
na wasiosikia kabisa. Wenye mdogo wa kusikia mwalimu anapaswa kuweka mbele ya
darasa na kwa wale wasiosikia kabisa vielelezo na teknolojia vifuatavyo
vinaweza kutumika:-
- Vielelezo na teknolojiamaono (Picha, chati, n. k)
- Vitu halisi (wataona, watagusa na kuonja)
- Lugha ya alama kwa wasiosikia
- Kufuatisha mdomo (lips reading)
©
KUNDI LA WASIOSEMA WALA KUSIKIA
Watu
ambao hawana uwezo wa kusema wala kusikia, mwalimu anashauriwa kutumia
vielelezo vifuatavyo:-
- Lugha ya ishara
- Vitu halisi kama vile miti, matunda, wanyama n.k.
- Picha mbalimbali Mfano, za wanyama, watu, mimea n.k.
TANBIHI:-
Watu kama wenye vipaji maalumu, walemavu wa miguu na wenye mtindio wa ubongo,
Vilelelezo vinavyoweza kutumika kwa watu hawa vitawiana
No comments:
Post a Comment