Vielelezo na teknolojia kwa ufundishaji na ujifunzaji
vimegawanyika katika aina kuu mbili.
1 Vielelezo na teknolojia asilia
2
Vielelezo na teknolojia kisasa
a)
VIELELEZO NA TEKNOLOJIA ASILIA
Ina maana ya zana au vifaa rahisi ambavyo huweza kupatikana au
kutengenezwa katika mazingira alimo mwalimu na wanafunzi kwa kutumia vitu
vilivyomo katika mazingira yao.Mfano,vitu halisi kama vile
matunda,samani,mimea,viumbe hai,nk.
Vifaa vya maumbo mbalimbali pia
huweza kutengenezwa kama vile vifani vya viumbe hai,maumbo yenye ukumbi kama
vik mche duara,mche mstatili,tufe nk.
SIFA ZA VIELELEZO
NA TEKNOLOJIA ASILIA
i.
Vinapatikana kwa urahisi
ii.
Havina gharama kubwa
iii.
Havihitaji maarifa ya ziada katika kuvitumia
iv.
Havitumii nishati ya umeme
vi.
Utengenezaji wake hujikita au hutokana na vitu
vinavyopatikana katika mazingira aliyomo mwalimu
na mwanafunzi
b)
VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KISASA
Hizi ni zana au vifaa vya kisasa ambavyo ni vigeni na havijazoeleka
katika kuvitengeza au kuvitumia.
Zana au vifaa hivi ni kama vile matumizi ya video,runinga,filamu,projekta
na kompyuta
SIFA ZA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KISASA
i.
Vina gharama
ii.
Vinahitaji nishati ya umeme
iii.
Vinahitaji maarifa na ujuzi wa kuvitumia
iv.
Havipatikani kwa urahisi
v.
Ni vigeni katika mazingira ya mwalimu na
mwanafunzi
vi.
Vinatumia sayansi na teknolojia ya hali ya juu katika matumizi yake.