Vielelezo na Teknolojia
kama somo linalojitegemea, linamlen ga
mkufunzi ili aweze kuwawezesha
wanachuo kupata ujuzi
na stadi za
kubuni, kufaragu a, kutengeneza
na kutumia zana au
vifaa na teknolojia
asilia na ile
ya kisasa katika
kufundishia na kujifunzia.
Lengo KUU la somo
hili ni
kuwaanda wanachuo wa
ualimu wa elimu
ya msingi ngazi
ya cheti waweze
kujifunza na kufundisha masomo mbalimbali kwa kutumia zana
zilizofaraguliwa au kutengenezwa.
Hapo awali, somo
la Vielelezo na
Teknolojia lilikuwa halifundishwi
chuoni kama somo
linalojitegemea. Badala yake
wakufunzi wa kila
somo walikuwa wakitoa maelekezo ambayo hayakumwezesha mwanachuo
kuandaa zana au
vifaa vya kufundishia. Mara nyingi maelekezo
hayo hayakuzingatia maarifa,
stadi, ujuzi na uwezo wa mwanachuo.
Somo hili litamwezesha
mwanachuo wa ualimu elimu ya msingi ngazi ya cheti kupata ujuzi, maarifa, stadi,
uwezo na mbinu
mbalimbali za kubuni,
kufaragua na kutengeneza zana au vif aa bora kwa ajili ya kumwezesha kufundisha kwa ufanisi.
Katika somo hili,
Vielelezo na Teknolojia
asilia ina maana
ya zana na
vifaa rahisi ambavyo huweza kupatikana
au kutengenezwa katika
mazingira alimo mwalimu
na
wanafunzi kwa kutumia
makunzi yaliyomo katika
mazingira hayo. Vitu
vingi halisi huweza
kupatikana kwenye mazingira
tulimo kama vile
matunda, samani, mimea,viumbe hai na
vingine vingi.Vifani
vya maumbo mbalimbali
pia huweza
kutengenezwa
katika mazingira kama
vile vifani vya
viumbe hai, maumbo
yenye ukumbi kama vile mche duara, mche mstatili, tufe na vingine
vin gi.Kwa upande
mwingine ‘Vielelezo na
Teknolojia kisasa ‘ina maana
ya zana au vifaa
vya kisasa ambavyo
ni vigeni na
havijazoeleka katika kuvitengeneza
au kuvitumia.
Zan a au vifaa hivi ni kama vile matumizi
ya video, luninga, filamu na ko mpyuta.
Mkufunzi unashauriwa
kuwa unapoongoza shu ghuli za
kujifunzia ni vema ufikirie na kuzingatia
masuala mtambuko.Mathalani
uzingatie jinsia kwenye
shughuli zinazohusu
vikundi vya kujifunza,usafi na utunzaji
wa mazingira kabla
na baada ya somo.Pia, zana au vifaa
vitakavyobuniwa, kufaraguliwa, au
kutengenezwa vihusishe
masuala ya afya
au magonjwa kama vile
Malaria, UKIMWI na mengineyo kwa kadri itakavyoonekana inafaa au kukidhi haja ya somo husika.
No comments:
Post a Comment