a) KUFARAGUA
Ni
ubunifu wa kutengeneza zana kwa kutumia vifaa au makunzi yasiyohalisi na
yanayopatikana katika mazingira husika.Ufaraguzi unaweza ukawa wa namna hizi;
- Kutumia kitu papo kwa papo kinyume na matumizi yake ya kawaida.Mfano,unapotumia penseli kama kishikizi katika kupigia mstari(hapa utakuwa umeitumia penseli kama rula.Ama vile,
- Kutumia malighafi/vifaa au makunzi zinazopatikana katika mazingira yetu husika(ama kwa kuokota au kuzitafuta) katika kutengeneza vifani mbalimbali(zana ) kwa gharama nafuu. Zana nyingi zinazobuniwa,faraguliwa na kutengenezwa hutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira yetu husika.Mfano unaweza;
(a) Kutengeneza vifani vya viumbe hai kwa
kutumia udongo(kufinyanga)
(b) Kutengeneza mpira kwa kutumia vitambaa
/makaratasi ya nailoni.(kushona)
(c) Kutengeneza kisu kwa kutumia miti(kuchonga)
nk.
b) MAKUNZI
Malighafi
zinazotumika katika kutengenezea kitu au zana.Vifaa hivi vinaweza vikawa vya
kuokota ama kununua.Mfano unaweza ukaokota mimea,maboksi,makopo nk.Pia unaweza ukanunua kadi za
manila nk.
c) ZANA MPITISHO
Ni
zana zinazotumika katika kupitishia maarifa yanayotolewa darasani katika swala zima la ufundishaji na ujifunzaji.Mfano
ubao wa chaki,Luninga nk.Ieleweke
kama si ubao ama chaki ndivyo vinavyopitisha maarifa,bali ni “Ubao wa chaki”,kwani
unaposema “Ubao “ni neno pana sana na linaweza likatumika katika miktadha
mbalimbali,kinyume na unaposema ubao wa chaki, hapa moja kwa moja utakuwa
umeiweka dhana hiyo katika muktadha wa ufundishaji na ujifunzaji.Pia chaki, haipitishi maarifa yoyote zaidi
ya kutumika katika kuandikia katika ubao.
d) KIVUNGE CHA SOMO
Kisanduku
cha mbao /bati kilichotengenezwa kwa
ajili ya kuhifadhia zana.Ifahamike
kuwa ,zipo baadhi ya zana ambazo ni rahisi kuharibika,na zingine ni
hatari kwa binadamu (kama viviminika vya kemikali),na baadhi ni gharama.Kwa
muktadha huu,mwalimu huna budi kuhifadhi zana zako katika mazingira yatakayokupelekea
kuvitumia tena baadaye na kutoleta madhara yoyote kwa watumiaji .
e) TEKNOLOJIA
Maarifa
ya sayansi yaliyowekwa kwenye matumizi ya vitu kama vile zana.Tunaamini kuwa
kwa Dunia ya sasa,kila eneo linaihusisha teknolojia katika uendeshaji wake.Kwa
mfano katika maswala ya biashara,kiuchumi nk. Sekta ya Elimu pia, hutumia
teknolojia katika uendeshaji wa shughuli zake. Matumizi ya teknolojia katika zana nayo yanachangia ubora wa elimu
yetu na kurahisisha swala zima la ufundishaji na ujifunzaji.Tunaweza kuona
namna ya zana mbalimbali za kisasa kwa mfano luninga,kompyuta, projekta, intarneti,
na mfumo wa mawasiliano ya kimkutano(teleconference system) zinatumika katika
kurahisisha tendo zima la ufundishaji na ujifunzaji.Matumizi haya ya teknolojia
yanahitaji ujuzi wa hali ya juu ili kuleta ufanisi katika suala zima la
ufundishaji na ujifunzaji.
f) KIFANI
Kitu
kinachofanana au kushabihana na kingine.Kuna aina kuu mbili za vifani;
a. Vifani vya viumbe hai(zana zilizotengenezwa kwa kuzingatia mifano ya maumbo mbalimbali ya
viumbe hai).Mfano,unaweza ukatengeneza mfano wa mtu kwa kutumia udongo na si kumtengeneza mtu
halisi(hivyo hushabiana na uhalisia wa kitu kilichotengenezwa) ama kuchora picha ya mfano wa simba,twiga
nk.Vivyo hivyo nazo zitawakilisha mfano au kushabiana na maumbo ya wanyama hao.
b. Maumbo yenye ukumbi kama vile mche
duara,mche mstatili,tufe na vingine vingi.Hapa ni zile zana zilizotengenezwa
kushabiana ama kufana na maumbo mbalimbali yenye ukumbi kama mche mduara.Mfano,unaweza
kutengeneza umbo la mstatili kwa kutumia boksi.Umbo hili litafanana/kushabiana
na umbo halisi la mstatili.
Naomba nisaidiwe aina nne za ubao wa kufundishia
ReplyDeleteZipo aina mbalimbali kama
Delete.ubao wa chaki-ule unaotumika zaidi madarasani ukiwa umepachikwa ukutani
.ubao wa fulana - Mara nyingi hutengenezwa kwa kutumia kipande cha blanketi. Watoto huweza kubainisha herufi au namba na zilizobandikwa chanacnana Dume na kuzipachika katika aina hizo za mbao.
.magnetic board - Ni zile mbao zenye mnato ambazo mwanafunzi anaweza kutumia stencil zilizoandaliwa kwa muundo wa vitu mbalimbali na kuzibandika katika mbao hizo wakati wa ujifunzaji.
.Ubao wa chaki
ReplyDelete.Ubao wa fulana (flannel board)
.magnetic board
Asanteni Sana!
ReplyDeleteSikujua ntajibiwa mapema..nmefurahi!
Naomba pia nisaidiwe hatua za kuchukua wakati unataka kutumia radio kama zana darasani
ReplyDeleteMambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kutumia ubao wa chaki
ReplyDeleteNaomba nisaidiwe tofauti kati ya chati na mabango
DeleteMambo ya kuzingatia wakati was kutumia ubao:
ReplyDelete-hakikisha kuwa ubao hauna maandishi mengine
-gawa ubao kwa kuzingatia ukubwa wake, standard huwa ni sehemu tatu
-wakati was kuandika usiwape mgongo wanafunzi simama upande
-wakati was kuandika usiwe karibu sana wala mbali sana,sm 30 toka ukutani na mguu wako
-unapoandika usilaze shingo au kichwa utapindisha mistari
- andika ubaoni kwa kuzingatia kimo chako
-tumia rula kwa kazi zote za ubao
Chaki za ranging zitumike kuchorea michoro na kupiga mistari
-Futa ubao baada ya kumaliza kazi ya ubao nk.
Rejea,TET,(2000) mitaala na zana za
kujifunzia,TET,Dar es salaam65-69.
Naomba kuuliza zana mafunzo Ni zipi na zana msingi Ni zipi?
ReplyDeleteNaomba kujua makundi ya vielelezo na teknolojia
ReplyDeleteYapo 3
Deletekundi la v/t maono
Masikizi
Masikizi-maono
Naomba kusaidiwa aina nne za ubao
ReplyDeleteNaomba kujua faida ya kutumia zana za kisasa katika kufundisha na kujifunzia
ReplyDeleteNaomba kusaidiwa kutambua sifa za makunzi boraa
ReplyDeleteNaomba kusaidiwa tofauti Kati ya vielelezo natekinolojia maono na makundi mengine
ReplyDelete