WELCOME NOTE

WELCOME NOTE

PICHA

PICHA

TANGAZO

Thursday, August 23, 2012

MALENGO YA SOMO LA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA


Baada ya kujifunza somo la vielelezo na teknolojia mwanachuo anatakiwa  aweze:
a) Kukuza ubunifu wa kuandaa vielelezo na teknolojia maono,        masikizi na masikizi-maono.
b) Kutambua aina mbalimbali za vielelezo na teknolojia katika kubuni,kufaragu a, kutengeneza na kutumia kwa kufundishia na kujifunzia.
c)Kubainisha sifa za kuzingatia k atika utengenezaji wa vielelezo na teknolojia bora na fanisi.
d) Kubainisha aina za vielelezo na teknolojia bora na fanisi.
e) Kueleza njia mbalimbali za utunzaji na usalama wa vielelezo na teknolojia.
f)  Kutumia aina mbalimbali za utunzaji na usalama wa vielelezo na teknolojia.

Monday, August 6, 2012

KARIBUNI KATIKA BLOG YA IDARA YA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA

Kwa mujibu wa Uongozi wa chuo cha Ualimu Mhonda,ningependa kuwakaribisha wana Vielelezo na tEKNOLOJIA ,NCHINI NA DUNIANI kote ili kupata habari mbalimbali zinazohusiana na somo hili la VIELELEZO NA TEKNOLOJIA.
Yapo mambo mengi ambayo tutashirikaiana katika blog hii,kupitia kona ya kupeana habari n.k.
Kama utakuwa na maswali mbalimbali tumia kona hiyo kwa kupata majibu kutoka watu mbalimbalimbali duniani.
Yeyote ambaye atakuwa na majibu sahihi kUhusiana na maswali yatayoulizwa,usisite kulijibu swali hilo moja kwa moja katika kona yetu ya kupeana habari.
Zingatia kutumia email iliyokuwa sahihi,na epuka kutumia lugha za mtaani katika blog hii.
Naamini mwalimu ni kioo cha Taifa,hivyo ni vizuri tukajiheshimu ili kuonesha mfano wa kuigwa katika jamii.
Tumia google transalate katika kutafsiri matini ya lugha mbalimbali na kubadilisa katika lugha yako husika
Kwa maoni na ushauri zaidi tuandikie kupitia email yetu idarayavielelezo@gmail.com
TUKISHIRIKIANA PAMOJA TWAWEZA KUWA WAALIMU BORA WA KUBUNI,KUFARAGUA NA KUTENGENEZA ZANA BORA  ZA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI KATIKA MASOMO YETU MBALIMBALI YA MCHEPUO! 
KARIBUNI WOTE!!!!!!